Timu ya Jeshi zaendelea kutesa Mashindano ya Netibali Dodoma
Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma
Mashindano ya ligi daraja la kwanza Netibali ngazi ya taifa yameendelea kutimua vumbi ndani ya uwanja CCM Jamhuri jijini Dodoma, ambapo katika mchezo wa kwanza Jiji Tanga wameshinda kwa magoli 48, dhidi ya Jiji Dodoma.
Mchezo wa pili JKT Makutopola wameshinda mabao 56, dhidi ya 24 ya Smart Queens, na JKT Mbweni wakashinda 60, dhidi ya 22 ya Coca cola Kwanza ya Dar es saalam, wakati Jeshi Stars wakishinda mabao 52, dhidi ya 31 ya Eagles.
Na kwa upande wa wanaume Bright ya Dodoma wakashinda magoli 24, dhidi ya 19 ya Smart Boys ya Dar es saalam.
Katibu wa CHANETA taifa Judith Ilunda ameiambia Muungwana Blog, kuwa mashindano hayo yataendelea leo, august 30, saa mbili na nusu asubuhi kwa TAMISEMI Dodoma dhidi ya Jiji Dodoma, Jiji Tanga dhidi ya JKT Makutupola.
Wakati JKT Mbweni dhidi ya Eagles na mchana Jiji Arusha dhidi ya Jeshi Stars, na Coca cola kwanza watacheza na Smart Queens.
Akataja timu zinazoshiriki mashindano hayo “Timu zinazoshiriki mashindano hayo kwa upande wa wanawake ni TAMISEMI, Coca Cola kwanza, Jiji Tanga, Jiji Dodoma, Smart Queens, JKT Mbweni, Jeshi Stars, Eagle, JKT Makutopola na Jiji Arusha” amesema Judith.
Kwa upande wa wanaume amezitaja kuwa ni Smart Boys, Bright, Muungano na hapa Kazi tu na mashindano hayo yalianza August 28, na yanatarajiwa kufikia kikomo Septemba 8, mwaka huu.

Comments
Post a Comment