Bocco awafunda wachezaji wenzake
NAHODHA WA SIMBA, JOHN BOCCO
Simba katika mchezo huo ilifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 na hivyo kujiweka katika mazingira mazuri yakufuzu kwa hatua inayofuata ya michuano hiyo.
Akizungumza na gazeti ili, Bocco, alisema kwa sasa ni kama wamecheza dakika 45 za kwanza na dakika 45 za pili watazicheza ugenini hivyo ni lazima wajipange kumaliza mchezo huo.
“kazi bado haijaisha, tunatakiwa kujipanga na kuweka akilini kuwa bado tuna kazi nzito mbele yetu, tunaenda kucheza ugenini na wenzetu watakuwa wamejipanga kujaribu kubadilisha matokeo,” alisema Bocco.
Aidha, alisema ili kusonga mbele wanapaswa kuwa na nidhamu ya mpira kwa dakika zote 90 watakazocheza ugenini.
“Kikubwa tutafuata maelekezo ya makocha wetu, na tutajitahidi kupambana kwa nguvu kuweza kusonga mbele,” alisema.
Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka nchini Kesho kwenda Eswatini (zamani ikijulikana kama Swaziland) tayari kwa mchezo huo.
Simba inahitaji sare au ushindi kuweza kusonga mbele na kama itapoteza mchezo huo isipoteze kwa zaidi ya mabao 3-0.
Comments
Post a Comment