BMT yaonya rushwa uchaguzi OBFT
BARAZA la michezo la taifa (BMT) limewaonya wajumbe watakaojitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la ngumi za wazi nchini (OBFT) kutoendekeza rushwa na badala yake wachague viongozi halali wenye uwezo wa kuinua mchezo wa ngumi.
Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo umepangwa kufanyika leo katika ukumbi wa Baraza la.michezo la taifa BMT.
Akizungumza na gazeti hili jana Katibu Mkuu wa BMT, Alex Nkenyenge alisema wapiga kura wanapaswa kuangalia umuhimu wa.mchezo na si maslahi binafsi.
Alisema kutokana na hilo wawakilishi wapiga kura kutoka vyama mbalimbali vya mchezo vya mkoa wanatakiwa kuwa makini katika zoezi hilo.
“tunaenda kwenye tukio muhimu la uchaguzi, niwaombe wapiga kura kutumia kura zao vizuri kwa kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuiongoza OBFT, na niwaambie tu wapiga kura na wagombea kuwa hatutafumbia macho vitendo vya rushwa,” alisema Nkenyenge.
Alisema jumla ya wagombea 18 watapata nafasi yakujieleza mbele ya wapiga kura nini watalifanyia Shirikisho hilo kutokana na kulegalega kwa sasa tofauti na ilivyokuwa awali.
Alisema uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki na hakuna atakeyonewa bali kura zawapiga kura ndizo zitakazoamua nani atakuwa kiongozi.
Aliwataja wagombea waliojitokeza kuchukua fomu ni pamoja na nafasi zao katika mabano ni Yono Levela na Musa Rwakatare,(Rais), nafasi ya Makamu wa Rais waliorejesha fomu ni Andrew Muhoja, Anil Kimabi, huku nafasi ya Katibu aliyerejesha fomu ni Robert Sululu na Lukelo Wililo.
Nafasi za wajumbe,waliorejesha fomu ni Zainabu Mbonde, Donath Antony, Asha Voniats, Mohamed Aboubakary, Riadha Samwel, Mafuru Mafuru na Samwel Samwel.

Comments
Post a Comment