Posts

Mikutano ya kampeni za mgombea Ubunge -Ludewa yatoa majibu ya kero ya Barabara iliyodumu kwa muda mrefu

Image
  Na Amiri Kikagalila, Njombe. Mbunge wa Jimbo la Ludewa  aliyepita bila kupingwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) wakili Msomi Joseph Kamonga ameendelea na mikutano ya kampeni za Kumuombea kura Rais Dkt John Pombe Magufuli na madiwani wa CCM ikiwa zimebaki Siku 16 kuelekea Kufanyika kwa Uchaguzi mkuu nchini Tanzania hapo Oktoba 28, 2020. Kamonga akiwa katika kata ya Madilu wilayani Ludewa amewashukuru Wananchi wa eneo hilo kwa kukiamini Chama cha Mapinduzi na kumpitisha yeye  bila kupingwa kuwa mbunge wa jimbo la Ludewa na amewaahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabiri ikiwemo swala la Barabara. ''Ndugu zangu nimekuja kusema Asante sana,Jambo la pili nimekuja kuwaombea kura viongozi wa CCM, Tumekuja kumuombea kura Rais wetu Mpendwa Dkt,John Pombe Magufuli,tunamuombea kura Magufuli kwa ujasiri kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya kwenye taifa letu ni Rais wa kipekee mfano pekee mwaka jana aliweka utaratibu wa Kusikiliza Changamoto za wafanyabishara mbalim...

Naibu kamishna wa uhifdhi utalii na huduma za biashara atembelea vituo vinavyosimamiwa na TAWA Mkoani Tabora

Image
NA FARIDA SAIDY. Naibu Kamishna Bw.Imani Nkuwi amefanya ziara ya kikazi katika vituo vilivyo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) vilivyopo Mkoani Tabora na kuzungumza na watumishi wa vituo vya Kanda Dhidi ya Ujangili ya Magharibi (KDU), Pori la Akiba la Ugalla, Pori la Akiba Luganzo Tongwe, na  Pori la Akiba Wembere Ziara  hiyo iliyofanyika tarehe 12.10.2020 pamoja na mambo mengine Naibu Kamishna Nkuwi alitoa ufafanuzi kwa watumishi hao kuhusu mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na Serikali katika Shirika pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakibili watumishi kwenye vituo vyao. Aidha, alitumia vikao hivyo kuwahimiza watumishi kufanya kazi kwa uzalendo, ueledi na kudumisha upendo miongoni mwao ili kuiwezesha TAWA kufikia malengo yake,huku akisisitiza kuzingatia Tunu za TAWA zilizoanishwa katika mpango kazi wao. Naibu Kamishna Nkuwi alitoa ufafanuzi kwa watumishi kuhusu mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na Serikali katika Taasisi za Uhifadhi ziliz...

Trump arejea kwenye kampeni baada ya kupona COVID-19

Image
Rais Donald Trump wa Marekani amerejea tena kwenye kampeni za uchaguzi mkuu kwa kufanya mkutano wa kwanza jimboni Florida siku kadhaa tangu alipogundulika na maambukizi ya virusi vya corona. Rais Trump aliwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la wazi huko Sanford; Florida bila ya kuvaa barakoa. Mkutano wa kampeni mjini Florida,  jimbo ambalo ni muhimu kwa Trump kushinda, unafungua njia ya mikutano zaidi iliyopangwa kufanyika wiki hii kwenye majimbo ya Pennsylvania, Iowa na North Carolina.  Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake waliosimama bega kwa bega wengi wakiwa bila barakoa, Trump amesema afya yake imeimarika na yuko huru kukutana tena na wapiga kura bila ya kuwa na wasiwasi wowote.  "Nimetiwa nguvu kwa maombi yenu na nimefarijika kwa uungaji wenu mkono. Tunaungwa mkono vya kutosha. Na tuko hapa lakini tunaenda kukamilisha, tutalifanya taifa hili kuwa kubwa kuliko ilivyokuwa hapo kabla." alisema rais Trump. Trump anayewania muhula wa pili katika uchagu...

Tetesi za soka kimataifa

Image
Manchester United imeweka mipango ya kumsainisha kiungo wa Rennes na Ufaransa Eduardo Camavinga, 17, iwapo mfaransa mwenzie Paul Pogba, 27, ataamua kuondoka Old Trafford. (Sport Witness) Uhamisho wa mshambuliaji wa Algeria Said Benrahma wa £25m kutoka Brentford kwenda West Ham uko hatarini kuvunjika, ambapo wapiga nyundo hao wamejielekeza zaidi kwa mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Josh King, 28. Crystal Palace huenda ikapeleka ofa ya lala salama kumnasa Benrahma, 25. (Mirror) Manchester City itajaribu tena kumsajili mlinzi wa kushoto wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico, 28, mwezi January. (Sun) Tottenham huenda ikarejesha nia yake ya kumsajili mlinzi wa kati wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar, 25, mwezi January. (Team Talk) Fulham wako katika hatua nzuri ya mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Huddersfield na Uholanzi Terence Kongolo, 26. (Football Insider) Wachezaji kadhaa wa Manchester United wameeleza masikitiko yao ya namna hali inavyomwendea mlinda mlango w...

MAGAZETI YA LEO 13/10/2020

Image
 

CHUO CHA TUMAINI JIPYA IRINGA KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO

Image
    Mkuu wa chuo cha afya na sayansi chirikishi tumaini jipya kilichopo  mafinga mjini mkoani iringa  chenye usajili wa baraza la taifa elimu ya ufundi nacte no hs/ 144 anawatangazia nafasi za masomo kwa mwaka  wa masaomo 2020/2021 kwa  kozi  zifuatazo Ordinary diploma in clinical medicine(  clinical officer) miaka mitatu technician certificate in clinical medicine(clinical assisstance)miaka miwili.           Mwombaji awe ufaulu wa alama ( D ) kwa masomo ya fizikia chemia na biologia Ordinary diploma in clinical medicine upgrading  ( mwaka moja) sifa awe amemaliza na kufaulu technician certificate in clinical medicine.    Pia chuo kina nafasi za kuhamia mwaka wa masomo 2020/2021, kwa wanafunzi wa  mwaka wa pili na mwaka wa tatu Maombi hufanyika chuoni kwa idhini ya nacte kwa mawasiliano fika chuoni tumaini jipya au piga simu  0756916610 / 0764986544 / 0762251717 Chuo kina mazingiza tu...

Kampuni 21 za nunua korosho RUNALI, bosi wa CBT na DC watema cheche

Image
Na Ahmad Mmow, Lindi.   Kampuni 21 zimenunua kilo 2,854,008 za korosho katika chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, kupitia mnada wa kwanza kwa msimu wa 2020/2021 uliofanyika kwenye viwanja vya ofisi kuu ya chama cha RUNALI iliyopo mjini Nachingwea.  Katika mnada huo ambao ulikuwa tofauti na minada ya misimu iliyopita kwa korosho kununuliwa kwa mifumo miwili tofauti ( mtandao kupitia soko la bidhaa,TMX na barua za kawaida ndani ya boksi la zabuni) ilishuhudiwa bei 82 tofauti zilizoombewa na kampuni hizo kununua zao hilo.  Ambapo kampuni zilizofanikiwa zimenunua kwa bei ya juu ya shilingi 2,555 na bei ya chini shilingi 2,422 kwa kila kilo moja.   Korosho zilizonunuliwa zipo katika maghala  yaliyopo katika wilaya za  Nachingwea na Ruangwa. Ambapo katika  ghala la Lipande, wilayani Ruangwa ambalo korosho zake zilinunuliwa kwa bei ya shilingi 2,395 hadi 2,345 lina kilo 580363.   Katika ghala Lindi farmes lililopo wilayani Nachingwe...