Posts

Ufaransa yatoa wito kwa jeshi la mapinduzi nchini Mali ''uharakisha'' ubadilishanaji wa mamlaka

Image
Ufaransa leo imetoa wito kwa jeshi la mapinduzi nchini Mali ''kuharakisha'' maandalizi ya kurejesha uongozi kwa raia baada ya mapinduzi ya mwezi huu na kuonya kuwa mzozo wa kisiasa utawanufaisha wanamgambo. Mapinduzi hayo dhidi ya serikali ya rais Ibrahim Boubakar Keita yaliishtua Ufaransa ambayo ni mshirika wa Mali inayohofia kuwa hali ya kukosa udhibiti nchini humo itahujumu kampeini za kijeshi dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali katika eneo la Sahel lililoko Afrika Magharibi. Waziri wa majeshi wa Ufaransa Florence Parly ameliambia shirika moja la habari la Ufaransa kuwa ubadalishanaji huo wa uongozi unapaswa kufanywa haraka katika muda wa miezi michache na kwamba iwapo hatua hiyo haitachukuliwa, athari itakayokuwa ni kuwanufaisha wanamgambo hao kwasababu hutumia udhaifu wa serikali na Mali kwa sasa ni taifa dhaifu. Maeneo mengi ya ngome ya Mali yako nje ya udhibiti wa serikali kuu na miaka kadhaa ya mapigano imeshindwa kumaliza shughuli za wanamgambo hao amba...

VIDEO: Hamonize ashuka kikomandoo taifa, atembea juu ya kamba

Image
Msanii wa bongo fleva, Harmonize amefanya suprise kwa wanachama na wapenzi wa mpira baada ya kutua uwanjani kwa staili ya kikomandoo huku akitembea juu ya kamba. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Mizinga ya Israeli yalenga Hamas baada ya mashambulizi ya mabofu kutoka Gaza

Image
Jeshi nchini Israeli limesema leo kuwa limeshambulia ngome za kundi la Hamas katika ukanda wa Gaza huku mashambulizi ya Palestina yanayoongezeka yakiendelea licha ya juhudi za amani za kimataifa. Katika taarifa iliyotolewa mapema leo, jeshi hilo limesema kumekuwa na mashambulizi ya milipuko ya angani na ya moto Kusini mwa nchi hiyo siku ya Jumamosi na kwamba kwa kujibu matukio hayo, makombora yalirushwa katika vituo vya kijeshi vya kundi la wanamgambo la Hamas katika eneo la Kusini la ukanda wa Gaza.Hata hivyo hakuna ripoti ya majeruhi iliyotolewa. Israeli imekuwa ikishambulia ukanda wa Gaza karibu kila siku tangu Agosti 6 kujibu vifaa vya mashambulizi ya moto na mara kadhaa makombora yanayorushwa kuvuka mpaka. Ujumbe wa Misri umekuwa ukiwasiliana na pande zote mbili kujaribu kuchochea kurejelewa upya kwa mkataba usiokuwa rasmi wa amani ambao Israeli imejitolea kulegeza vikwazo vya muda wa miaka 13 dhidi ya Gaza ili kurejesha utulivu katika eneo la mpaka.

Mzee wa Utopolo awapa onyo kali Manara na Manula

Image
Hizi ni tambo za wiki ya Wananchi wa Klabu ya Yanga ambayo inakamilishwa leo kwa kutambulisha wachezaji wapya, jezi mpya na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya nchini Burundi kuanzia 11:00 Jioni kwenye Uwanja wa Benjamin William Mkapa. Kamera za EATV & EA Radio Digital imempata shabiki kindakindaki wa timu hiyo Mzee wa Utopolo ambaye amefunguka matarajio ya timu yake, pia amempa onyo kipa wa Simba Aishi Manula na msemaji wa timu hiyo Haji Manara juu ya uwezo wa mchezaji wao mpya Carlinhos. "Historia ya mchezaji wetu Carlinhos inavyosemekana makipa wengi waliokuwa wanajaribu kufuata mipira yake wameishia Hospitali, ukijaribu kufuata mipira yake mikononi basi ujue viganja hauna, namuonya sana Aishi Manula akijaribu kufuata mipira ya huyu bwana basi ni Hospitali moja kwa moja" amesema Mzee wa Utopolo Akizungumzia onyo lake kwa Haji Manara Mzee wa Utopolo ameongeza kusema "Ujumbe wangu kwa Manara namuomba jumapili akae kwenye station ashuhudie wanan...

Rais wa Afghanistan ateuwa kundi la upatanisho kwa mazungumzo ya amani

Image
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani ametangaza wajumbe na uongozi ulioteuliwa wa baraza kuu la maridhiano ya kitaifa nchini humo katika juhudi za kusukuma mbele mazungumzo ya amani. Agizo la rais lililotolewa hapo jana jioni, limesema kuwa lengo la uteuzi wa wanasiasa hao wa kiwango cha kitaifa lilikuwa kutafuta makubaliano ya kitaifa ya kuongoza mazungumzo hayo ya amani. Wanasiasa wa ngazi za juu, viongozi wa vyama vya kisiasa na viongozi maarufu wa kidini ni miongoni mwa wanachama wa baraza hilo. Agizo hilo la rais lililipa baraza hilo kuu jukumu la kuunda mkutano mkuu wa baraza hilo katika muda wa wiki moja kwa kuhusisha watu wa matabaka mbali mbali nchini humo. Ni mwanamke mmoja pekee aliyeteuliwa katika baraza hilo kuu ambalo pia lilikosa uwakilishi wa vijana hali iliyoibua shtuma kali.Baraza hilo kuu la maridhiano ya kitaifa ni taasisi tofauti inayosimamia kundi la wanachama 21 wa mazungumzo ya amani lililoundwa ili kuwezesha mazungumzo ya moja kwa moja na kundi la Taliban. ...

Boti lililowabeba watafuta hifadhi wa Uturuki lawasili nchini Ugiriki

Image
Maboti mawili ya kuvulia samaki yaliowabeba watu wanaotafuta hifadhi 26 kutoka Uturuki yamewasili katika kisiwa cha Ugiriki cha Chios, walinzi wa Pwani ya Ugiriki wamesema hii leo. Kundi hilo lililowajumuisha watoto, liliokolewa na walinzi hao lilipokaribia ufuo huo hapo jana. Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Politischios nchini humo, raia hao wa Uturuki walikuwa wanatafuta hifadhi ya kisiasa nchini Ugiriki wakidai kuteswa na serikali ya rais Recep Tayyip Erdogan. Abiria wawili walitoboa mashimo katika boti lilipokuwa likikaribia kisiwa hicho kuchochea juhudi za uokoaji. Wawili hao walikamatwa baadaye. Kundi la watu hao lilipimwa virusi vya corona na kuhamishiwa katika kituo cha karantini cha Lefkonia. Visa wa raia wa Uturuki wengi wao wakiwa watumishi wa umma na maafisa wa kijeshi wanaofika katika visiwa vya Ugiriki na kuingia nchini humo kupitia mpaka katika mto Evros vimeripotiwa tangu mwaka 2016 baada ya kushindwa kwa jaribio la kuipindua serikali ya rais Erdogan.

Wataalamu wa afya walalamika kuhusu Trump kupuuza sheria za corona

Image
Wataalamu wa masuala ya afya ya umma siku ya Ijumaa walielezea wasiwasi wao kuhusu tukio la mkutano wa chama cha Republican katika ikulu ya White House iliyoongozwa na rais Donald Trump ambapo baadhi ya wageni waalikwa 1500 hawakuvaa barakoa na kusema huenda baadhi ya wageni hao walileta bila kukusudia na kueneza virusi vya corona. Dkt Leana Wen, daktari wa masuala ya dharura na Profesa wa afya ya umma katika chuo kikuu cha George Washington, amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba kulikuwa na watu waliokuwa na maambukizi ya virusi hivyo lakini hawafahamu hali zao. Viti vilipangwa umbali wa inchi chache badala ya futi 6 zilizopendekezwa na kuwaacha washirika hao na nafasi ndogo ya kutimiza sharti la kujiweka kando na watu. Ni wageni waliotarajiwa kuwa karibu na Trump na naibu wa rais Mike Pence ndio waliotarajiwa kupimwa ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi hivyo.