Posts

VIDEO: Full Video Kilichotokea Mbowe, Matiko kukosa dhamana

Image
Mahakama Kuu ya Tanzania imesitisha kusikiliza rufaa ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini,Esther Matiko hadi rufaa ya upande wa mashtaka itakaposikilizwa Mahakama ya Rufani ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya kusikiliza rufaa hiyo. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI..........USISAHAU KUSUBSCRIBE............ 

Nedy Music afunguka kuhusu kufanya kolabo na Yvonne Chakachaka

Image
Msanii wa muziki Bongo, Nedy Music amejibu iwapo alikutana na Yvonne Chakachaka walipanga kufanya wimbo wowote. Nedy kwenye mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema waliongea kawaida ila mambo ya kufanya wimbo pamoja bado. "Sisi tunasema tupo bize lakini mama naye yupo bize sana, ni mtu ana ratiba za kutosha na tumekutana mara mbili tumezungumza lakini hatukupa ule muda mzuri wa mimi kuweza kuyazungumza mengi," amesema Nedy. Nedy Music na Yvonne Chakachaka walikutana nchini Ghana wiki iliyopita kwenye utoaji wa tuzo za All Africa Music Awards (AFRIMA).

VIDEO: Yafahamu makaburi yaliyogeuzwa kuwa vitanda vya kufanyia mapenzi Dar

Image
Eneo la maziko ya makabuli ya Maganga lililopo kata ya 14 Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam, liligeuka na kuwa kichaka cha uhalifu baada ya baadhi ya wakazi wa eneo hilo kugeuza kufanyia matumizi yaliyo kinyume na eneo hilo.  Ambapo walikua wakitumia kuvutia bangi, kuhifadhi silaha Huku wakiyatumia makaburi hayo kuwa kama vitanda vya kufanyia mapenzi na hivyo kuwalazimu baadhi ya waumini ya dini ya Kiislam kuungana na kuchangishana fedha na kujenga ukuta ambao umezunguka eneo hilo. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE 

Lady Jaydee azungumzia wasanii kuandaa show zao wenyewe

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Lady Jaydee amefunguka mara baada ya  baadhi ya wasanii kuanza kuandaa show zao wenyewe. "Kuna umuhimu kwa sababu inapotokea mtu mwingine hawezi kukupa kazi wewe mwenyewe unaweza kujipa kazi lakini si kila msanii anaweza akaandaa show na sio kila msanii anaweza akafanya show akajaza," amesema Lady Jaydee.  "Kwa hiyo kuna tofauti hapo na wasilaumiwe watu ambao hawawezi kuandaa show lakini ni jambo zuri kwa sababu tutawapa hata waandaaji changamoto kuwa wasituchukulie poa," amesema kwenye Mahojiano na The Playlist ya Times FM .

Wafanyabiashara wa mafuta Uganda watolewa wasiwasi

Image
Serikali imewahakikishia wafanyabiashara wa mafuta kutoka Uganda kuwa imejipanga kutatua  changamoto zote zilizopo kwenye usafirishaji ili kupunguza gharama za uchukuzi  kati ya Tanzania na nchi hiyo. Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, amesema hayo wakati wa kikao maalum kilichowakutanisha wafanyabiashara wa Mafuta wa Uganda na taasisi za Uchukuzi za Tanzania na kusema kuwa Serikali inatekeleza hayo kwa kuboresha miundombinu ili kuvutia wafanyabiashara wengi zaidi “Niwahakikishie kuwa changamoto zote zilizoainishwa baada ya majumuisho ya ziara yenu ya siku 5 nchini tutazifanyia kazi”, amesema Naibu Waziri  Nditiye. Aidha, Naibu Waziri Nditiye ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ikiwemo upanuzi wa bandari,ukarabati wa reli na ukarabati wa meli ili mizigo inayokwenda Uganda kupitia bandari ya Dar es Salaam ifike kwa wakati. Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya Meli, Eric Hamis amesema mpaka sasa tayari wa...

Watoto 80 wenye matatizo ya moyo wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji JKCI

Image
Jumla ya watoto 80 wenye matatizo ya moyo wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya matibabu itakayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mradi wa Little Heart wa nchini Saud Arabia ambao ni moja ya mradi wa Afya ulioko ndani ya Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao Makuu yake mjini Londoni nchini Uingereza. Matibabu hayo yatahusisha upasuaji wa moyo wa kufungua kifua kwa watoto wenye matatizo makubwa na upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo kwenye paja kwa watoto wenye matatizo yasiyohitaji upasuaji wa kufungua kifua. Watoto wanaotarajiwa kufanyiwa matibabu hayo katika kambi hiyo wameshafika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kufanyiwa uchunguzi wa awali tayari kwa kulazwa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji huo. Kambi hiyo ya siku nane inatarajia kuanza kesho tarehe 1 Desemba 2018 hadi tarehe 8 Desemba 2018 kwa kutoa matibabu ya kina kwa watoto wote w...

PBZ yabadilisha mfumo mpya wa Kibenki

Image
Benki ya Watu wa Zanzibar(PBZ), imesema imepata mafanikio makubwa baada yakubadilisha mfumo mpya wa kibenki ujilikanao 'Banks' ikiwemo huduma ya kutumafedha katika akaunti za ndani za PBZ na nje ya nchi. Akizungumza leo na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo,Juma Hafidhi alisema mfumo huo umeondoa changamoto zilizokuwepo ambazo zilikuwazikiwapatia usumbufu wateja na kwamba kwa sasa imeleta mafanikiomakubwa ambapo awali kabla ya mfumo huo katika ufungaji wa hesabu kwasiku ilikuwa ikichukua muda wa masaa matatu lakini kwa sasa dakika 10. Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa baada ya kubadilisha mfumo huo sasa mtu ambaye ni mteja wa PBZ kutuma pe sa kwa mtu ambae ni si mteja wa benki hiyo na kuweza kuchukua fedha yake katika tawi lolote la benki hiyo. "Mfumo huu pia unamwezesha mtu kutuma fedha kwa mteja wa PBZ na kumpelekea mtu ambae si mteja wa benki yetu ambae ataweza kutowafedha katika ATM za benkiya PBZ,"alisema Mkurugenzi huyo Katika maelezo yake ...