Borell: EU ina wasiwasi na mapigano mapya ya Nagorono Karabakh


Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borell ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na ripoti za ukiukaji makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya mataifa jirani yaliyo hasimu ya Armenia na Azerbaijan ya kuwania udhibiti wa jimbo la Nagorno Karabakh.

Taarifa iliyotolewa na mwanadiplomasia huyo wa Umoja wa Ulaya, imesema kanda hiyo inatiwa shaka na operesheni za kijeshi zinazoendelea ikiwemo zinazohujumu maeneo ya makaazi na kuwalenga raia.

Taarifa hiyo Borell imetolewa baada ya kuvunjika kwa sehemu fulani makubaliano ya kusitisha mapigano kufuatia kuzuka makabiliano mapya huku kila upande ukiulaumu mwingine kuhusiana na kilichotokea.

Borell amesema Umoja wa Ulaya unatoa wito wa pande hasimu kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano na kuanza mazungumzo chini ya upatanishi wa kundi liitwalo OSCE Minsk linaloongoza juhudi za kumaliza mzozo wa Karabakh.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato