Wakazi wa eneo la Mkunwa kurasimishiwa maeneo yao
Na Faruku Ngonyani, Mtwara.
Timu ya Wataalamu wa ardhi kutoka Halmashsuri ya Wilaya ya Mtwara wameanza rasmi mchakato wa upimaji eneo la Mkunwa ambao kwa Sasa ni Makao Makuu ya Halmashauri hiyo.
Zozi la Upimaji wa eneo hilo likiwa na lengo la kurasimisha makazi ya wananchi sambamba na kuupanga mji huo wa Mkunwa.
Kwa upande wa wananchi wamefurahishwa na zoezi hilo ambapo mara baada ya kumalizika kwa zoezo la Urasimishaji wa mji huo kutawawezesha wananchi kutambua na kujua mipaka ya maeneo wanayoishi.
Kata ya Mkunwa ipo katika Mpango wa Mji kabambe wa Mtwara (Mtwara Master Plan) ambapo kuanza kwa zoezi hilo ni maandalizi katika kuendelea kutekeleza Mpango huo Kimkakati Mkoani Mtwara
Comments
Post a Comment