Viongozi wa Azerbaijan na Armenia wakataa kuzungumza


Viongozi wa Azerbaijan na Armenia wamepuuzia pendekezo la mazungumzo ya amani baina yao, huku kila mmoja akimshutumu mwengine kwa kuzuwia mapatano juu ya jimbo linalowaniwa la Nagorno-Karabakh, ambako watu kadhaa wameshauawa na kujeruhiwa ndani ya kipindi cha siku tatu za mapigano makali. 


Katika tukio la karibuni kabisa, Arnmenia imesema ndege yake moja ya kijeshi iliangushwa na ndege nyengine ya kijeshi ya Uturuki, ambayo ni mshirika mkubwa wa Azerbaijan, na kumuua rubani wake. 


Uturuki na Azerbaijan zimekanusha taarifa hiyo. Jumuiya ya kimataifa inazitaka pande hizo mbili kufanya mazungumzo ya kukomesha mzozo huo wa miongo kadhaa baina ya mataifa hayo yaliyowahi kuwa sehemu ya Shirikisho la Jamhuri za Kisovieti kwenye Milima ya Caucasus. 


Nagorno-Karabakh inatambuliwa kimataifa kuwa sehemu ya Azerbaijan, lakini imekuwa chini ya udhibiti wa vikosi vya waasi wanaoungwa mkono na Armenia tangu mwaka 1994. 


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana lilitoa tamko linazozitaka pande hizo mbili kurejea kwenye meza ya mazungumzo bila masharti yoyote.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato