Tetesi za soka kimataifa


 Manchester United imeanza mazungumzo na Barcelona kuhusu kumnyakua kwa mkopo mshambuliaji Mfaransa Ousmane Dembele 23. (Mirror)

Tottenham wamemaliza makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Benfica Carlos Vinicius,25, kwa mkopo, ambaye gharama ya kuondoka kwake ni kiasi cha pauni milioni 89 kwa mujibu wa kufungu cha mkataba wake. (Mail)

Wakala wa mshambuliaji wa Real Madrid Luka Jovic,22, amesema raia huyo wa Serbia anataka kujiunga na Manchester United, huku inter Milan na Roma zikimtolea macho pia. (Star)

Liverpool wanajiandaa kukubali ofa ya pauni milioni 23 kutoka Sheffield kwa ajili ya mshambuliaji Rhian Brewster. (Sun)

Wekundu hao pia wamejiandaa kufaidika na kiungo wa zamani Philippe Coutinho wa Barcelona, ​​na kitita cha pauni milioni 4.4 ikiwa Mbrazili huyo,28 atacheza mechi nyingine 14. (Mirror)

Manchester United wamekataa kuhusishwa kwao na taarifa za kumsajili Ainsley Maitland-Niles,23, ambaye anaweza kucheza nafasi ya ulinzi na kiungo wa kati kutoka Arsenal. (Manchester Evening News)

Arsenal wako kwenye mazungumzo ya kumtoa kwa mkopo kiungo wao wa kati Matteo Guendouzi kwenda Marseille. (Telefoot via Express)

Chelsea inaweza kuongeza wachezaji wa kuondoka kwenye klabu hiyo kwa kumuuza mlinzi Mhispania Marcos Alsonso, 29, beki wa kati Antonio Rudiger, 27, na kiungo wa kati Ruben Loftus-Cheek, 24 kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili. (Star)

Newcastle United wanajiandaa kupambana na Valencia katika mbio za kumsajili mlinzi wa Juventus Daniele Rugani ambaye pia anahusishwa na taarifa za kutakiwa na Fulham, West Ham na Sevilla. ( Sportitalia)

Washika bunduki hao pia wameongeza jitihada za kumshawishi kiungo wa kati anayekipiga Lyon Houssem Aouar,22, huku rais wa klabu Jean- Michel Aulas akikiri kuwa wanaweza ''kuwapoteza wachezaji wawili'' kabla ya muda wa mwisho. (Metro)

Ofa ya hivi karibuni ya Roma kwa beki wa kati wa Manchester United Chris Smalling ya pauni milioni 10.9 pamoja na marupurupu mengine ya thamani ya pauni milioni 2.7 inafikiliwa na klabu hiyo ya Old Trafford. (Mail)

Aston villa wako mbioni kumsaini beki wa kati Kerr Smith ,15, kutoka Dundee United. (Dundee Telegraph)



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato