Siku ya wazee duniani: Jamii iwajibike kuwatunza
Oktoba 1 kila mwaka, ni Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani inayotambulika na Umoja wa Mataifa katika Azimio namba 45/106 la mwaka 1990
-
Siku hii ni mahususi kwa ajili ya kutambua Haki na Changamoto wanazokumbana nazo wazee katika jamii. Tanzania maadhimisho haya mwaka huu yatafanyika kimkoa
-
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Naphtali Ng'ondi amesema Serikali imefanikiwa kupunguza mauaji ya wazee nchini kutoka wazee zaidi ya 500 miaka mitano iliyopita, na mwaka 2019 mauaji 74 tu yaliripotiwa
-
Aidha, amesema wameongeza idadi ya wazee wanaopatiwa Huduma za Afya bure na pia, wameboresha Vituo vya Kuwatunza Wazee nchini
Comments
Post a Comment