Mujata yaonya uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Shirika la muungano wa jamii Tanzania(MUJATA) limeitaka jamii ya Tanzania kutunza amani iliyopo nchini hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika 28 oktoba mwaka huu.


Hayo yalisemwa na katibu mkuu wa shirika hilo ngazi ya Taifa Hekima Malila wakati wa kikao cha shirika hilo ngazi ya kanda uliofanyika katika mkoa wa Njombe na kushirikisha wajumbe kutoka nyanda za juu kusini.


Alisema jamii inapaswa kutambua kuwa amani iliyopo hapa nchini imeenziwa kwa muda mmrefu na waasisi wa nchi hii na kutuachia ambapo mpaka sasa imeendelea kuwepo.


Alisema jamii inapaswa kutambua kuwa amani iliyoopo nchini haikununuliwa popote pale hivyo endapo jamii itaruhusu ipotee itatugharimu katika kuirudisha amani hiyo.


"Tumezoea kuona tunaishi kwa amani , tunaabudu kwa amani na hata kazi zetu za maendeleo zimekuwa zikiendelea na nchi yetu kuelekea uchumi wa kati kwasababu kuna amani" Alisema Hekima.


Alisema jamii inapaswa kutambua kuwa yenyewe ina jukumu kubwa la kulinda amani ya nchi hii hivyo shirika limejipanga kwa namna ya kipekee kuhakikisha jamii kwenye maeneo yao inapatiwa elimu namna ya kulinda amani iliyopo.


Aidha aliitaka jamii kushirikiana na vyombo vya dola kufichua na kutoa taarifa za kiharifu na kichochezi ambazo kwa kiasi kikubwa zinaweza kuligawa taifa hili.


Nae mwakilishi wa vyombo vya dola ndani ya shirika la Mujata Agnes Wiliam amesema jeshi la polisi limekuwa likipata ushirikiano wa karibu kiutendaji kutoka MUJATA kwenda serikalini au jeshi la polisi.


Alisema jeshi la polisi kupitia MUJATA limekuwa likipata taarifa kutoka chini kabisa kwa maana ya jamii nzima ambazo zimekuwa zikitumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo utatuzi wa migogoro, taarifa za uhalifu na wahalifu mbaxo zinakwenda jeshi la polisi na kufanyiwa kazi.


"Ushirikiano kutoka MUJATA umetupa ufanisi mkubwa katika utendaji wa kazi hasa pale tunapopata taarifa kutoka chini moja kwa moja zinakuja jeshi.la polisi hivyo tunaishukuru MUJATA kwa ushirikiano huo" Alisema Agnes.


Aidha amelishukuru jeshi la polisi mkoa wa Njombe kwa kuhakikisha kuwa maandalizi ya kufanyika kikao hicho yanafanikiwa ikiwa ni sambamba na kupatiwa usafiri wa kuwatoa sehemu moja kuelekea nyingine.


Mwenyekiti wa vijana MUJATA taifa Victor Lazaro alisema vijana wanapaswa kutambua kuwa wao ndiyo walioshikiria nguzo ya amani ya taifa hili ingawa wanasiasa wengi wamekuwa wakiwatumia vijana vibaya kwa kuwashirikisha katika vitendi viovu vya uvunjifu wa amani katika taifa hii hasa kutokana na hali ya uchumi wa vijana.


"Sisi kama vijana tumelikemea hili katika kila kona ya Tanzania na kusema hatutakubaliana na mwanasiasa yeyote ambaye atawashawishi vijana kuwa cha vurugu au uvunjifu wa amani" Alisema Victor.


Mjumbe wa MUJATA kutokea mkoa wa Njombe Frida Mbembate aliwataka wanawake kuwa makini kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu kwa kuhakikisha wanailinda amani iliyopo bila ya kujali tofauti ya itikadi zao za vyama vyama siasa.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato