Mdahalo wa Urais: Ukweli wa madai ya Trump na Biden

 


Rais Trump na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden wamekabiliana kwa mara ya kwanza katika mdahalo wa kwanza kati ya mitatu itakayopeperushwa kwa njia ya televisheni kabla ya uchaguzi wa urais utakaofanyika Novemba.


Wakati wa mdahalo huo uliochukua dakika 90, wagombea hao walikabiliana kwa kila jambo walilokuwa wanazungumzia kuanzia uchumi hadi namna ya kukabiliana na janga la virusi vya corona.


Kitengo cha Reality Check BBC kimechambua baadhi ya madai hayo.

Trump: "Tumeimarisha uchumi kwa kiasi kikubwa katika historia"

Uamuzi: Huo sio ukweli - kumekuwa na wakati katika historia ya Marekani ambapo uchumi umeimarika zaidi.


Kabla ya mlipuko wa virusi vya corona, rais Trump alidai kwamba uchumi umeimarika kuliko kipindi kingine chochote kile.


Ni kweli uchumi ulikuwa unafanya vizuri kabla ya janga la corona - ikiwa ni kile kilichokuwa kinaendelea wakati wa utawala wa Obama - lakini kuna wakati ambapo uchumi uliimarika zaidi.


Biden: "Tuna asilimia 4 ya idadi ya watu duniani, [lakini] asilimia 20 wamekufa"


Uamuzi: Hili huenda lina ukweli kwa kiasi fulani. Lakini ukiangalia idadi ya vifo ikilinganishwa kwa mtu mmoja mmoja, kuna idadi ya nchi ambazo ziko vibaya zaidi kuliko Marekani.


Bwana Biden amekosoa utawala wa Bwana Trump jinsi ulivyoshughulikia ugonjwa wa Covid- 19.


Kulingana na idadi hiyo, ni kweli. Marekani ina idadi ya watu milioni 328 ambayo ni asilimia 4 tu kati ya watu bilioni 7.7 duniani.


Kumekuwa na vifo 205,942 vilivyorekodiwa Marekani kutokana na virusi vya corona, kulingana na Chuo Kikuu cha John Hopkins. Idadi ya vifo vilivyorekodiwa duniani ni 1,004,808.


Katika hili, Marekani inahesabu asilimia 20 ya vifo kutokana na Covid-19 duniani, ingawa kuna tofauti kuhusu namna nchi zinavyoredi idadi idadi hiyo.



Trump: ongezeko la upigaji kura kwa njia ya posta utasababisha "ulaghai ambao haujawahi kushuhudiwa"


Ukweli: utafiti haujabaini ushahidi wa kutokea kwa ulaghai ingawa kumekuwa na visa kidogo.


Kutokana na janga la virusi vya corona, idadi kubwa ya wapiga kura inatarajiwa kupiga kura kwa njia ya posta katika uchaguzi wa mwaka huu.


Rais ameonya mara kadhaa hili litasababisha kutokea kwa kiwango kikubwa cha udanganyifu.


Kumekuwa na visa kidogo vya udanganyifu ikiwemo mifano ya hivi karibuni huko North Caroline na New Jersey.


Septemba, Idara ya sheria Marekani ilitoa taarifa kuhusu tukio la Pennsylvania ambapo "kura 9 za wanajeshi zilipatikana na kuharibiwa na kusema saba kati ya kura hizo zilikuwa zimepigwa kumuunga mkono Rais Donald Trump".


Lakini licha ya matukio hayo, utafiti uliofanywa mara kadhaa haujaonesha mapungufu makubwa ya kukithiri kwa udanyanyifu.


Kiwango cha ulaghai kwenye upigaji kura kwa jumla nchini Marekani ni kati ya asilimia 0.00004% na asilimia 0.0009, kulingana na utafiti wa mwaka 2017 wa kituo cha Sheria cha Brennan.


Biden: "watu milioni 100 [Marekani] wanaugua magonjwa yanayowaweka katika hatari"

Uamuzi: hakuna jibu la moja kwa moja.


Wagombea hao walikabiliana kuhusu watu wangapi Marekani wenye magonjwa yanayowaweka katika hatari ambako kunaweza kusababisha baadhi yao wasiweze kupata huduma ya bima ya matibabu.


Bwana Biden alisema kulikuwa na watu milioni 100 ambao tayari wana maradhi mengine lakini rais Trump alisema kuwa idadi hiyo ni uongo mtupu.


Ni wangapi waliopo? Hakuna jibu sahihi.


Kulingana na Idara ya Afya na Huduma Marekani, kati ya watu milioni 50 na 129 ambao sio wazee tayari wana matatizo ya afya.


Mashirika mengine yana idadi tofauti. Kituo cha Maendeleo Marekani kinaamini idadi hiyo ni ya juu, watu milioni 135 wakiwa chini ya umri wa miaka 65.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato