Mahakama yasitisha mgomo katika hospitali kubwa zaidi Afrika Mashariki
Mahakama ya wafanyakazi nchini Kenya imesitisha mgomo wa uliyoitishwa na wafanyakazi wa hospitali Kuu ya Kenyatta, KNH.
Jaji Maureen Onyango ameagiza zaidi ya wafanyakazi 5,000 kurejea kazini wakisubiri kusikizwa kwa kesi.
Muungano wa wafanyakazi unaowawakilisa wauguzi, madaktari na wafanya kazi wengine katika hospitali hiyo umeagizwa kufika mbele ya mahakama hiyo Oktoba tarehe 6.
Wafanyakazi wanalalamikia kucheleweshwa kwa malipo yao ya mishahara na marupurupu yaliyoboreshwa.
Comments
Post a Comment