Magufuli aahidi upanuzi bandari ya Manda wilayani Ludewa-Njombe

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Chama cha mapinduzi CCM kupitia kwa mgombea wao wa nafasi ya,Rais ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli,wameahidi kupanua bandari ya Manda wilayani Ludewa mkoani Njombe ili kurahisisha usafiri kwenye ziwa Nyasa.


Magufuli ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni zake mjini Makambako wakati akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho kwa mwaka 2015-2020 na namna watakavyotekeleza Ilani yao 2020-2025


"Tumepanga kupanua bandari ya Manda iliyopo wilaya ya Ludewa ili kurahisisha usafiri katika ziwa Nyasa kama mnavyofahamu kwenye miaka mitano iliyopita tumejenga Meli mpya tatu kwenye ziwa Nyasa kwa ghalama ya shilingi bilioni 20.4 tunataka ziwe zinatua mpaka Manda kwenye Bandari" alisema Magufuli.


Vile vile amesema wako mbioni kukamilisha ujenzi wa Chuo cha Ufundi (VETA) kinachojengwa Shaurimoyo wilayani Ludewa mkoani humo ili kuwezesha vijana kupata mafunzo ya ufundi waweze kujiajili na kuajiliwa.


Mgombea wa Ubunge jimbo la Ludewa,Wakili Joseph Kamonga,amesema ni shuhuda  wa ujenzi wa miradi mbali mbali ya serikali kwa kuwa alikuwa mtumishi wa serikali na anaamini Chama cha Mapinduzi kitakwenda kukamilisha miradi inayoendelea katika jimbo hilo.


“Mimi nilikuwa mtumishi wa serikali nimeshuhudia ni jinsi gani Rais Magufuli alivyo boresha nidhamu serikalini,ninaomba ifikapo tarehe 28 watu wote twende tumpigie kura Dkt,John Pombe Magufuli ikiwa ni shukrani kwa aliyotendea taifa letu”Alisema Joseph Kamonga


                 



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato