YANGA yapania kulipa kisasi kwa KAGERA SUGAR
KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa anaamini wachezaji wake watalipa kisasi cha kufungwa mabao 3-0 na Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara walipokutana mara ya kwanza Uwanja wa Uhuru.
Mchezo huo wa Ligi ulichezwa Januari 15,2020 ulikuwa ni wa kwanza kwa Eymael kukaa kwenye benchi la ufundi akichukua nafasi ya Mwinyi Zahera
Akizungumza Eymael amesema kuwa ana waamini vijana wake watalipa kisasi kwenye mechi ya leo hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambalo ni muhimu kwao.
"Walitufunga mchezo uliopita kwenye ligi ila sio huku kwenye Shirikisho, wachezaji wangu wapo vizuri na ninaamini watatumia nafasi ya kulipa kisasi ili kuendelea kulinda heshima ya uwezo wao," amesema.
Mshindi wa mchezo wa leo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba na Azam FC hatua ya nusu fainali.
Comments
Post a Comment