Virusi vya corona: Raia wa mataifa 'salama' 14 ndio watakaoruhusiwa kuingia EU
Umoja wa ulaya (EU) umetaja majina ya nchi 14 ambazo wananchi wake wanadaiwa kuwa salama kuruhusiwa kuingia katika nchi zake kuanzia Julai, mosi , licha ya mlipuko uliopo lakini Marekani, Brazil na China hazipo katika orodha hiyo.
Mataifa yaliyotajwa ni pamoja na Australia, Canada, Japan, Morocco na South Korea.
Muungano wa Ulaya upo tayari kuiongeza China katika orodha kama tu serikali yake China itatoa ruhusa sawa kwa wasafiri wa umoja wa ulaya, mwanadiplomasia anasema.
Makatazo katika mipaka ya Umoja wa ulaya imeondolewa kwa wasafiri ambao ni raia wa Umoja wa ulaya kusafiri ndani ya ukanda wao.
Sheria zilizowekwa dhidi ya wasafiri wa Uingereza ziko tofauti na makubaliano ya Brexit.
Wananchi wa Uingereza wanachukuliwa sawa na raia wa Muungano wa Ulaya mpaka mwisho wa kipindi cha mpito Desemba, 31.
Katika orodha ya sasa, maeneo salama ambayo yanaweza kuongezwa ni nchi za Algeria, Australia, Canada, Georgia, Japan, Montenegro, Morocco, New Zealand, Rwanda, Serbia, South Korea, Thailand, Tunisia na Uruguay.
Kwa sasa Uingereza inafanya majadiliano na mataifa kadhaa ambayo ni wanachama wa Umoja wa ulaya, kuona namna ambavyo virusi vya corona vinaweza kutozuia kabisa mapumziko ya wakati wa msimu wa watalii unaowaajiri mamilioni ya watu.
Jumanne majira ya mchana, Umoja wa Ulaya itarasimisha nchi gani inapaswa kuhukumiwa kuwa salama au hapana .
Mataifa mengi ya Umoja wa ulaya - yapata 55% ya mataifa ya Umoja wa mataifa, ambayo ni sawa na 65% ya idadi ya watu wa Umoja wa ulaya ambao wako kwenye orodha.
Kuna mgawanyiko kati yao kama vile Uhispania - inataka kukuza utalii lakini inataka kujionyesha salama licha ya ugonjwa wa corona kuathiri nchi hiyo kwa ukubwa na nchi nyingine ni Ugiriki,na Ureno, ambazo zote zinategemea utalii lakini wanaogopa virusi.
Comments
Post a Comment