Viongozi wawili CHADEMA wahamia TLP


Wanachama wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Tanzania Labour (TLP), huku wakitoa sababu mbalimbali zilizowafanya wafikie uamuzi huo.

Wanachama hao wamepokewa na kukabidhiwa kadi za TLP na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Agustine Lyatonga Mrema, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya chama hicho Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa wanachama hao ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), Bibiana Benedict Dule Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, ambaye amesema amejiunga na chama hicho kutokana na msimamo wake wa kumuunga mkono wazi wazi Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Mwingine ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Ulinzi wa Chadema Kanda ya Serengeti Oscar Kaijage kutoka mkoani Shinyanga, ambaye pamoja na mambo mengine amesema amejiunga na chama hicho kutokana na kuvutiwa na utendaji kazi wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kueleza kuwa kwa hali ya nchi ilivyo kumpinga Rais Magufuli ni kupinga maendeleo.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato