Kocha wa Yanga amtimua Bernard Morrison kambini

Kocha Mkuu wa Yanga SC Luc Eymael ameeleza masikitiko yake na kuamua kumuondoa kambini mchezaji Bernard Morrison aliyemleta Yanga January 2020 wakati anajiunga nao, Morrison kaondolewa kwa vitendo vya utovu wa nidhamu.

“Nidhamu aliyoionesha kambini asubuhi hii (jana) nimeamua kumuondoa kambini sababu ya tabia yake sitaki kuzungumzia sana bahati mbaya sijui kapatwa na nini, toka nimerudi (likizo ya Corona) sijui kijana wangu (Morrison) niliyemleta hapa kapatwa na nini”

“Nimeongea nae sana muda wote sijui hata kimemtokea nini hapa kama nilivyosema niliamua asubuhi hii (jana) kumuondoa kambini na club itatoa taarifa rasmi kuhusiana na hili”

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato