Jinsi wadukuzi walivyotapeli chuo kikuu Marekani $1.14m, Marekani
Taasisi ya ngazi ya juu ya utafiti nchini Marekani inayofanyia kazi tiba ya ugonjwa wa corona imekiri kuwa iliwalipa matapeli dola milioni 1.14 sawa na (£910,000) kama kikombozi katika tukio ambalo lilishuhudiwa na BBC.
Genge la majambazi la Netwalker lilivamia Chuo Kikuu cha California San Francisco (UCSF) Juni mosi 2020.
Maafisa wa idara ya teknolojia walizima kompyuta zote za chuo hicho katika harakati za kuzuia kuenea kwa shambulio hilo la kimtandao.
Chanzo cha habari ambacho hakikutaka kutajwa kiliifahamisha BBC na kuiwezesha kufuatilia majadiliano ya kikombozi katika njia ya moja kwa moja mtandaoni na wa wadukuzi hao.
Wataalamu wa usalama wa mtandao wanasema majadiliano kama hayo sasa yanafanyika karibu kila sehemu duniani - wakati mwingine kinahusisha kiwango kikubwa cha fedha - kinyume na ushauri wa kisheria unaotolewa na mashirika ya upelelzi ikiwemo FBI, Europol na kituo cha kitaifa cha Uingereza kinachoshughulikia masuala ya usalama mtandaoni.
Netwalker pekee ndio ambayo imehusishwa na uvamizi wa kimtandao dhidi ya vyuo vingine vikuu viwili katika kipindi cha mize miwili iliyopita.
Ukifuatilia kwa karibu, mtandao wa Netwalker unafanana na mtandao wa kawaida unaotoa huduma kwa wateja ulio na kitengo cha maswali yanayoulizwa mara kwa mara (FAQ), ofa ya "bure" ya huduma wanazotoa pamoja na sehemu ya mawasiliano ya moja kwa moja na wateja.
Laking pia kuna sehemu ambayo inaonesha saa inayoendana na wakati wadukuzi wanapoendesha shughuli zao na ambayo huongeza muda mara mbili na kiwango cha fedha wanazoitisha kama kikombozi, ama kufuta data walizokusanya baada ya kudukua akaunti za wateja wao.
Wanaoambwa kujiunga na mtandao huo - kupitia barua pepe au kuachiwa ujumbe unaowataka kulipa kikombozi katika kompyuta iliyodukuliwa - Chuo Kikuu cha California San Francisco (UCSF) kilipata jumbe, huu uliotumwa Juni 5.
Comments
Post a Comment