Dkt Avemaria awashangaa wale wanaotembea na vyeti
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt Avemaria Semakafu, amewashangaa wale walimu walioweka vyeti vyao ndani kwa miaka minne bila kutafuta nafasi ya kujitolea kwenye shule zenye uhitaji na badala yake wamekaa kusubiri ajira kutoka Serikalini.
Dkt Semakafu ametoa kauli hiyo leo Juni 30, 2020, kuwa walimu wengi wako radhi kutembea na vyeti vyao makwapani na si kujitolea, ambapo kwa sasa Serikali imeelekeza nguvu zake katika kulipa madeni ya walimu.
"Umetoka kuongelea hapa Shule ya Usese ina upungufu mkubwa wa Walimu, lakini kuna walimu huu ni mwaka wa nne yuko mtaani anatembea na cheti kwapani, hata ile kusema aende kujitolea na kuonesha uzalendo wake katika shule zenye uhitaji, lakini mimi niseme sasa kwanza Serikali inamalizia mzigo wa madeni ya walimu ya huko nyuma" amesema Dkt Avemaria.
Aidha Dkt Avemaria ameongeza kuwa, "Mwalimu akikata tamaa ujue ni yule ambaye hajitambua, maana mwenye kujitambua anajua tunaenda wapi na ualimu ni harakati, na tuhakikishe tunatumia harakati za ualimu wetu kuleta maendeleo".
Comments
Post a Comment