Posts

VIDEO:Madiwani CHADEMA wavuruga kikao "DC amevunja kanuni"

Image
Madiwani wa halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe wanaotokana na chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wamesababisha kikao cha baraza la madiwani,kutulia kwa muda kutokana na kuomba taarifa wakilalamika kwa madai kuwa mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amevunja kanuni za kikao baada ya kukaribishwa na kutoa salamu za serikali kwa zaidi ya dakika 10. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

MAGAZETI YA LEO 31/1/2020

Image

Dhamana kwa kesi ya uhujumu uchumi yajadiriwa bungeni

Image
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amesema kwa kuwa kesi za uhujumu uchumi hazina dhamana ipo haja sasa kwa wabunge na Bunge kutunga sheria ya marekebisho na kubadilisha pale ambapo itaona panafaa. Hayo ameyabainisha leo Januari 30, 2020, Jijini Dodoma, kwenye Mkutano wa 18, Bunge la 11, Kikao cha Tatu, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Sabrina Sungura, lililohoji sababu ya vijana wengi wakiwemo kina Tito magoti kukutwa na kesi za uhujumu uchumi, na kukaa mahabusu muda mrefu, je Bunge halioni kama ni muda mwafaka sasa kufanya mabadiliko ya sheria ya uhujumu uchumi ili kuwapa nafasi Majaji na Mahakimu ambao wamekuwa wakiendesha kesi hizi ili waweze kutoa dhamana. "Kuhusu suala la mabadiliko ya sheria ya uhujumu uchumi, nadhani ni Mamlaka ya Bunge hili kutunga sheria na kubadilisha pale ambapo inaona panafaa, na kama kuna utaratibu mwingine wa kuleta hoja binafsi ili sheria hii ya uhujumu uchumi, iweze kubadilishwa" amejibu Mhandi...

IGP Sirro akutana na Mkuu wa jeshi la polisi Zimbabwe na kufanya naye mazungumzo

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Tanzania inanufaika kiulinzi na usalama kutokana na kuwa mjumbe wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa nchi za ukanda wa Kusini mwa Afrika (SARPCCO). IGP Sirro ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kikao na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Polisi Zimbabwe, TG Matanga ambaye yupo nchini kwa ziara maalum. IGP Sirro amesema kuwa kutokana na kuwa mjumbe wa shirikisho hilo, Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuia na kudhibiti makosa yanayovuka mipaka yakiwemo makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu, wizi wa magari na dawa za kulevya. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho hilo ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Zimbabwe, Kamishna Jenerali TG Matanga, amesema yupo nchini kwa ziara maalum ya kufanya tahmini ya utekelezaji wa maazimio ya INTERPOL pamoja na maazimio ya SARPCCO.

Serikali yawatoa hofu wakulima nchini "Hakuna uthibitisho wa kitaalam uwepo wa nzige"

Image
Serikali imewatoa hofu wakulima nchini kuwa hakuna taarifa za uthibitisho wa uwepo wadudu hatari aina ya Nzige wa Jangwani walioripotiwa katika nchi za jirani. Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ametoa kauli hiyo jana (29.01.2020) wakati alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dodoma na kusema Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kufuatiliaji viashiria vya uwepo wa Nzige wa Jangwani (Locust Desert). “Hadi sasa hakuna uthibitisho wa kitaalam kuhusu uwepo wa Nzige wa Jangwani nchini Tanzania” alisisitiza Waziri Hasunga Alibainisha wazi kuwa Serikali imejipanga kuwadhibiti nzige hao endapo wataingia nchini na tayari ina lita 7,000 za viuatilifu kwa ajili ya tahadhari ya kukabiliana na tishio hilo na ununuzi wa viuatilifu vingine zaidi unaendelea kufanyika. Alisema Wizara yake inaendelea kuchukua tahadhali kuhakikisha visumbufu vya mazao ya kilimo kama Nzige Wekundu, Ndege waharibifu wa nafaka aina ya Kwelea kwelea, panya na Kiwavijeshi Vamizi zinaripotiwa na kudh...

JNIA yajipanga kukabiliana na Virusi vya homa ya Corona

Image
Kitengo cha Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza, kilichopo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), kimejipanga kukabiliana na wagonjwa watakaobainika kuwa na virusi vya homa ya Corona, vilivyoanzia nchini China. Daktari George Ndaki, ambaye ni Mdhibiti wa Magonjwa ya Kuambukiza wa JNIA, leo amesema Wizara ya Afya imekabiliana na ugonjwa huo na tayari imefunga mashine tano zinazotumia komputa zinazopima joto la mwili la abiria bila kujitambua, na mashine sita za mkononi, ambazo abiria anapimwa endapo ataonekana kuwa na joto kali zaidi. Amesema mashine moja imefungwa kwenye Jengo la Watu Mashuhuri (VIP) ,nyingine imefungwa Jengo la Pili la abiria na tatu zipo jengo la Tatu la abiria, wakati za mkono zimeganywa kwenye majengo hayo. Dkt Ndaki amesema wataalam wa afya wanaokuwa kwenye mashine zinazotumia komputa wanamtambua abiria mwenye jotokali mara anapopita mbele ya kamera, na endapo litab...

DC Rajabu aitaka jamii kupanda miti kuzuia Mmomonyoko wa Ardhi

Image
Na Thabit Madai, Zanzibar. MKUU wa  Wilaya ya Kaskazini  ‘B’ Rajab Ali Rajab ameitaka jamii kupanda miti ya kudumu katika maeneo yenye mmong’onyoko wa ardhi katika kipindi cha mvua ili kukabiliana na mabadiliko ya tabiaya nchi. Amesema   njia pekee ya kukabiliana na mabadiliko ya tabiayanchi  ni kupanda miti pamoja na kujiepusha kukata miti ovyo hususan kwa kutumia misumeno ya moto ambayo imeonekana kuwa ndio chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira. Akizungumza  mara baada ya kushiriki zoezi la upandaji miti  katika kijiji cha  mwanakombo mkuu huyo wa wilaya amesema uzoefu unaonesha kuwa kipindi hiki ni kipindi cha kiangazi  lakini kumekuwepo na barka ya mvua hivyo ni vyema kwa jamii kuitumia fursa hii kwa kupanda miti ya kudumu. Aidha  Rajab amewataka Masheha kusimamia miti iliyopandwa katika maeneo yao ili iweze kukua vizuri na  lengo la Serikali la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi liweze kufikiwa. Hata  hi...