Posts

Bada ya kumchapa Tinampay, amtaka Manny Pacquiao na Amir Khan

Image
Baada ya bondia Hassan Mwakinyo usiku wa jana kumchapa Arnel Tinampay wa ufilipino kwa pointi, ametangaza kutamani kuwaona Manny Pacquiao na Amir Khan wanatua bongo kuzichapa. Akiongea na Azam TV, baada ya kumalizika kwa pambano hilo, Mwakinyo alisema anatamani Manny Pacquiao na Amir Khan waje Tanzania acheze nao maana haamini kama kuna utofauti wa ngumi.   "Huu ni mwanzo tu, tunamtaka Manny Pacquiao na Amir Khan waje Tanzania hapa tucheze nao. Mimi siamini kama kunautofauti wa ngumi, ngumi nilizocheza mimi ndio alizocheza Mfilipino ingawa mimi nipo Tanga na yeye yupo Ufilipino kwa Manny Pacquiao," amesema Mwakinyo. Pia Mwakinyo amefunguka sababu ya kutofanya vizuri kwenye pambano lake la jana dhidi ya Tinampay huku akitaja sababu kubwa iliyomuangusha ni gloves alizovaa sio zile ambazo amezoea kupigana nazo.  "Niliamini kwenye ufiti wangu hajakutana na mtu anayeweza kupiga. Nimegundua kitu kinachombeba siyo bondia mkali bali ni mvumilivu sana. Hata mimi sija...

Madiwani wasusia kikao, Kisa halmashauri kuhamishiwa kijiji walichokikataa

Image
Na Hamisi Abdulrahmani, Masasi   Madiwani Watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara wakiongozwa na Makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo, wamesusia kikao cha baraza na kutoka nje ya ukumbi kwa madai kuwa hawakubaliani na maamuzi ya serikali kuhamishia ofisi za halmashauri katika kata ya Mbuyuni.   Madiwani hao wamedai kuwa mwenyekiti na mkurugenzi wameshindwa kutoa ufafunuzi sahihi na wakimaandishi kuwa ninani ambaye ametoa idhini ya ofisi za Halmashauri hiyo kuhamia kwenye kijiji cha hicho. Walisema maazimio ya madiwani kuhusu makao makuu ya ofisi za Halmashauri yaliamuliwa na madiwani wenyewe kuwa ofisi hizo zihamie katika mji mdogo wa Ndanda ambapo huduma nyingi za kijamii zipo ikiwemo umeme na ufasiri tofauti na Mbuyuni ambapo ofisi zimehamia kwa sasa. Akizunguma mara baada ya kutoka nje ya ukumbi makamu mwenyekiti  Halmashauri hiyo, Nestory Chilumba ambaye pia ni diwani kata ya Mwena, alisema ameamua kutoka nje kuungana na wenzake wa nne kut...

Waziri Prof. Mbarawa awapa somo Mameneja wa mamlaka za maji

Image
Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma. Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa amewataka Mameneja wa Mamlaka za maji kuhakikisha wanaongeza mitandao ya maji kwa wananchi sambamba na kuimarisha ukusanyaji wa mapato yatokanayo na matumizi ya maji kwa wananchi na taasisi mbalimbali. Pia amesema serikali imejipanga kuhakikisha wanatatua changamoto za maji katika maeneo mbalimbali hapa nchini, huku akiwataka wataalamu wa kusoma mita kufanya kazi kwa weredi kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuepuka kuhujumu mapato. Waziri Profesa Mbarawa ameyasema hayo akiwa katika  Mji mdogo wa Kibaigwa Wilayani Kongwa, Mkoani Dodoma, wakati akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Maji ya mji mdogo wa kibaigwa, katika ziara ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa katika Wilaya ya Kongwa. Amesema serikali imejipanga kuhakikisha wanamaliza tatizo la maji na  ni lazima Mamlaka zihakikishe zinaongeza mitandao ya maji kwa wananchi na kusimamia ukusanyaji wa mapato na hata sita kuwaondoa wale wanaozembea...

VIDEO: Prof. Mbarawa atingisha kiberiti , nitabadilisha viongozi mmoja baada ya mwengine

Image
WAziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa amesisitiza kuwa serikali imejipanga kutatua kero za maji huku akiwataka Wahandisi wa Mamlaka za Maji kuhakikisha wanaongeza mitandao ya maji kwa wananchi na kuwataka kusimamia ukusanyaji wa mapato yatokanayo na maji na kuwaonya wataalamu wa kusoma mita za maji kuhakikisha wanafanya kwa waaminifu TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBSCRIBE 

MAGAZETI YA LEO 30/11/2019

Image

Kocha wa Arsenal Unai Emery afurushwa kazi

Image
Kocha wa Arsenal Unai Emery amefutwa kazi baada ya kuongoza timu hiyo kwa kipindi cha miezi 18. Raia huyo wa Uhispania  ambaye awali alikuwa mkufunzi wa Paris St-Germain katika ligi ya Ufaransa na kushinda mataji matatu ya Europa akiwa na Sevilla, aliteuliwa kuwa mkufunzi wa Arsenal mwezi Mei 2018, akimrithi Arsene Wenger. Mahala pake patachukuliwa kwa muda mfupi na aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Freddie Ljungberg. Arsenal inasema kwamba uamuzi huo ulichukuliwa baada ya matokeo ya timu hiyo kushindwa kufikia kiwango kilichohitajika. Arsenal haijashinda katika mechi saba na ilipoteza 2-1 nyumbani dhidi ya klabu ya Ujerumani Eitracht Frankfurt katika ligi ya Europa siku ya Alhamisi.

Tundu Lissu atua Kenya, aeleza mipango ya kurejea Tanzania

Image
Mwanasiasa wa upinzani nchini na aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amesema atarejea Tanzania baada ya  marafiki zake kumhakikishia usalama wake. Ametoa kauli hiyo jana akihojiano na kituo cha televisheni cha KTN cha nchini Kenya baada ya kuulizwa kuhusu mpango wake wa kurejea nchini. “Hali ya usalama wangu bado si nzuri, nafikiri hakuna mtu anayetaka kuona narudi nyumbani kesho na keshokutwa ninapigwa risasi tena. Bado kuna vitisho vya aina hii,  watu wenye busara lazima wakae na kuangalia namna nzuri ya kufanya ili niweze kurudi nyumbani kuendelea na shughuli zangu lakini nikiwa salama.” asema. “Hizi jitihada zinafanywa na marafiki wa ndani na nje ya nchi kuhakikisha nakuwa salama kurudi Tanzania. Ikifika mahala wakasema usalama wangu utaangaliwa nitarudi nyumbani.” ameeleza. Mwanasheria mkuu huyo wa CHADEMA kwa sasa Lissu yupo Nairobi nchini Kenya. Ikumbukwe Septemba 7, 2017, Lissu alishambuliwa kwa risasi akiwa kwenye gari nje ya ...