Kamishna Mkuu TRA awapa neno wajumbe wa EARATC kuhusu maadili
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dkt. Edwin Mhede amesema kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hazina budi kutilia mkazo suala la maadili ili kujenga uelewa wa pamoja na kuwa na mikakati shirikishi ya kutokomeza vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa mamlaka za mapato vinavyokwamisha ukusanyaji mzuri wa mapato. Dkt. Mhede ameeleza hayo wakati akifungua mkutano wa 10 wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki (EARATC) kuhusu maadili unaoendelea Jijini Dodoma. Amefafanua kwamba, katika mkutano huo masuala mbalimbali yanajadiliwa zikiwemo fursa mbalimbali pamoja na changamoto kama vile masuala ya upitishaji wa mapato haramu mipakani pamoja na namna ya kushirikiana katika kutoa adhabu kwa wafanyaji makosa hayo. “Katika mkutano huu tunajadili masuala mbalimbali, mfano suala la maadili kama vile utovu wa nidhamu kwa watumishi wetu wa mamlaka za mapato, lakini pia tutaona namna ya kushirikishana katika kutoa adhabu kwa wafanyaji makosa katika ...