Posts

BREAKING: Watuhumiwa 467 waomba kukiri makosa ya uhujumu uchumi

Image
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema ofisi yake imepokea barua za watuhumiwa 467 wanaoomba kukiri makosa ya uhujumu uchumi na wapo tayari kurudisha fedha jumla ya Sh107.8 bilioni. DPP ameyasema hayo leo wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa Ushauri alioutoa wa kuwasamehe Watuhumiwa wa Uhujumu Uchumi walio tayari kutubu na kurejesha Fedha na Mali. Hata hivyo, Biswalo Mganga  amemuaomba Rais John Magufuli kuongeza siku tatu kwaajili ya kuwapa nafasi watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali. Hata hivyo Rais Magufuli ameongeza siku saba kuanzia leo Jumatatu Septemba 30, 2019  kwaajili ya kuwapa nafasi watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kumuandikia barua DPP ya kuomba kutubu na kurejesha fedha na mali.

Hizi hapa timu 16 zilizofuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Image
Hizi hapa timu 16 zilizofuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, CAF Champions League 1. 1° de Agosto (Angola) 2. USM Alger (Algeria) 3. Al-Ahly (Misri)🇪🇬 4. Wydad AC (Morocco) 5. Raja CA (Morocco) 6. Vita Club (DR Congo)  7. Etoile du Sahel (Tunisia) 8. Al-Hilal (Sudan) 9. JS Kabylie (Algeria) 10. Platinum (Zimbabwe) 11. Petro Luanda (Angola) 12. TP Mazembe (DR Congo) 13. Sundowns (Afrika Kusini)  14. ES Tunis (Tunisia)  15. Zamalek (Misri) 16. ZESCO (Zambia)

TPB yazindua tawi jipya Masasi

Image
Na Ahmad Mmow, Lindi Benki ya Posta Tanzania( TPB) imefungua tawi lake dogo jipya wilayani Masasi Mkoani Mtwara ili kutimiza dhamira ya benki hiyo ya kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi,hasa wale wanaoishi maeneo ya wilayani na vijijini katika mikoa ya kusini. Hafla ya uzinduzi wa tawi hilo jipya wilayani Masasi imefanyika jana wilayani hapo katika viwanja vya tawi la benki hiyo mpya maarufu kama mkuti mjini Masasi na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali. Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo kufanyika mtendaji kuu wa benki hiyo (CEO) Sabasaba Mongishi alisema kuwa wameamua kusongeza huduma za benki ya Tpb kwa wananchi wa wilaya ya Masasi. Alisema kwa muda mrefu wakazi wa wilaya hiyo na wilaya za jirani wamekuwa na kiu kubwa ya kupata huduma ya benki ya Posta Tanzania hivyo hitaji hilo sasa limepatiwa jawabu kwa kufungua tawi hilo jipya Masasi. Alisema tangu ianzishwe mwaka 1925 na sasa kutimiza miaka 94 imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kuongeza idadi ya mat...

Prof. Kabudi ampa Kongole Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amempa Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim kufuatia kitendo cha kutunukiwa Nishani ya Juu ya Urafiki ya Jamhuri ya Watu wa China nishani ambayo inamfanya Dkt. Salim kuwa mwafrika wa kwanza kupewa heshima na tuzo hiyo ya juu katika historia ya China. Prof. Palamagamba John Kabudi amesema Nishani aliyopewa Dkt. Salim Ahmed Salim anastahili na kuwataka Watanzania wanapopewa majukumu ya Kitaifa kuyafanya kwa uaminifu na uzalendo usiotiliwa mashaka kwakuwa mbali na kumpa muhusika sifa inaleta heshima kwa Taifa zima kama ilivyo kwa Dkt. Salim Ahmed Salim.

China yagundua eneo lenye mafuta Tani Bilioni 1

Image
Shirika la Taifa la Mafuta la China (CNPC) ambalo linaongoza kwa uzalishaji na usambazaji wa mafuta na gesi, limetafiti hifadhi mpya ya gesi na mafuta. Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo jana imesema, limegundua uwanja wa mafuta wenye tani bilioni 1 za mafuta katika eneo la kaskazini magharibi mwa China. Makamu rais wa Kampuni ya PetroChina, ambayo ni tawi la CNPC Li Luguang amesema, jumla ya tani 640,000 za mafuta zitazalishwa katika eneo hilo kwa mwaka huu, na litafikia tani milioni 3 kwa mwaka katika siku zijazo.

Kijiji cha Songosongo waishukuru na kuipongeza WWF

Image
Na Ahmad Mmow, Lindi Wananchi wa kijiji cha Songosongo katika wilaya ya Kilwa wamelipongeza na kulishukuru shirika la kimataifa la uhifadhi na utunzaji mazingira duniani(WWF) kwa uvumilivu uliosababisha waanze kufaidi matunda ya uvumilivu huo. Jana wakizungumza kwenye ufunguzi wa mwamba darasa, uliofanyika katika bahari ya Hindi katika kijiji hicho,  walisema shirika hilo lilikutana na vikwazo vingi wakati linaanza kutoa elimu kwa wananchi wa kijiji hicho ambao kazi kubwa inayowaingizia kipato ni uvuvi. Said Mgeni, ambaye ni diwani wa kata ya Songosongo alisema WWF lilipata upinzani  kutoka kwa wananchi wakati linaanza kutoa elimu kuhusu uhifadhi na usimamizi wa mazingira. Ikiwemo madhara ya uvuvi haramu na faida za uvuvi salama.  Alisema wananchi walipandikizwa dhana mbaya kwamba WWF iilitaka kujimilikisha maeneo. 4: Diwani huyo alisema vikwazo hivyo havikulikatisha tamaa shirika hilo,bali liliendelea kutoa elimu ambayo wananchi wameanza kunufaika nayo. ''Kwetu...

Walimu watakiwa kuacha kutumia Kilimo kama adhabu kwa wanafunzi

Image
Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba amewataka walimu wa shule za Msingi na Sekondari waache kutumia kilimo kama adhabu ya kuwapa wanafunzi wakati wanapokosea kwani inawajengea tafsiri mbaya kwa jamii na baadae wanapokuwa wanachukia kilimo. Mgumba alisema hayo wakati wa ziara yake wilayani Pangani ambapo alisema kwamba kuna tabia ambayo imejengeka kwa walimu hao kwamba mtoto anapokosea anaambiwa leo utakwenda kilima siku nzima, utakwenda kumwagilia hali ambayo inapelekea baadae wakikua wanakuwa hawahitaji kilimo kwa sababu awali waliona kama adhabu. Alisema kwamba hapana suala hilo sio jema na ndio maana wao wanasema kilimo ni ute wa mgongo lakini watafungamanisha kilimo na elimu ili watoto tokea anakuwa ajue kwamba nchi hii uchumi wake unategemea kilimo. “Hivyo ninapoambiwa niwe na tuta la mchicha sio adhabu bali ni sehemu ya kuniandaa kielimu nije kujitegemea au nije kuajiri wengine kwenye mashamba yao kwani bila kufanya hivyo tutakuwa tunaimba kitu kingine wakati uchumi wetu...