Posts

Namna ya kujaza nywele kwa njia za asili

Image
Namna ya kujaza nywele kwa njia za asili Kunamtu amenitumia swali juu ya nini afanye ili Nywele zake ndefu ambazo ni chache, zijae. Nataka kumwambia kwamba hilo linawezekana kwa kufanya yafuatayo. Chukua parachichi kubwa moja, asali vijiko vitatu na kiini cha yai. Osha nywele zako kwa shampoo na uzikaushe. Ponda ponda parachichi mpaka lilainike kabisa. Chukua vijiko vitatu vya asali na kiini cha yai kisha changanya yote kwa pamoja. Paka mchanganyiko huo kaa nao kwa muda wa dakika 15 kisha osha. Fanya hivyo kwa muda wa wiki moja hadi mbili na utaweza kuona matokeo mazuri katika nywele yako.

Mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuomba mkopo

Image
Kutokana na kipato cha watu wengi kutokutosheleza mahitaji yao, hujikuta wakilazimika kukopa. Wapo waliofanikiwa sana kwenye mipango yao kutokana na mikopo, lakini wapo pia waliofilisika kutokana na mikopo. Kwa hakika swala la mikopo linahitaji umakini mkubwa pamoja na mipango na mikakati stahiki ili lisije likakuingiza kwenye madeni yasiyokwisha. Ikiwa una mpango wa kukopa, basi fahamu mambo  muhimu ya kuzingatia kabla ya kuomba mkopo. 1. Bainisha uwezo wako wa kifedha Ili upate na utumie mkopo vyema, ni muhimu ufahamu uwezo wako wa kifedha. Ikiwa uwezo wako wa kifedha ni shilingi milioni moja, ukikopa mkopo wa bilioni 1 hutoweza kuupata wala kuurejesha. Hakikisha unatathimini kipato chako pamoja na uwezo wako wa kutumia pesa ili usije ukatumbukia kwenye madeni. 2. Andaa mpango wa matumizi na marejesho Watu wengi hushindwa kupata mkopo au kurejesha mkopo kutokana na kutokuwa na mpango mzuri wa matumizi na urejeshaji wa mkopo. Hakikisha kabla ya kukopa unaandaa mpan...

Unapotaka kufanikiwa kimaisha unatakiwa kukumbuka mambo haya

Image
Moja yachangamoto ambayo inawakabili watu wengi ni kwamba ni wazuri sana wa kusema kuliko kuchua hatua, hapa nina maana ya kwamba kila mmoja anapenda kuona matarajio yake yanatimia, hata hivyo kutokana na imani hiyo imepekelekea watu wengi sana kubaki na maisha yale yale kila siku. Unajua ni kwanini? Basi nakusihi ufuatane nami kwani nataka nikijuze siri ambayo watu wengi hawaijui juu ya upangaji wa malengo. Ipo hivi niliwahi kufanya uchunguzi mdogo katika kazi yangu ya uhamasishaji mahali fulani, moja ya maada ambayo nilikuwa naizungumzia siku hiyo ilikuwa inahusiana na jinsi gani unavyoweza kutimiza  malengo yako na kila mmoja ilionekana kufurahia somo hilo. Kila mmoja wetu ambaye ulikuwepo siku hiyo ilionekana dhairi anayo ndoto ambayo inasukuma kufikia kilele cha mafanikio. Ndipo nikachukua jukumu la kutaka kujua kila mmmoja aliyekuwepo siku hiyo ni nini ambacho anaadhamiria katika maisha yake? Kila mmoja alieleza kwa mapana kutoka na dhamira inavyomsukuma kutoka nafsini ...

Faida zitokanazo na kula uyoga kiafya

Image
Uyoga una vitamini na aina nyingi na madini. Virutubisho vilivyothibitishwa kuwemo kwenye uyoga ni pamoja na Vitamin B2, B3, B5, B6, B Complex pamoja na madini ya Potasiamu na Phosphorus. Virutubisho hivyo ni muhimu kwenye mwili wa binadamu katika kutoa na kuimarisha kinga ya kupambana na ‘wavamizi’ maradhi. Aidha, inaelezwa kuwa uyoga ni chanzo kingine kizuri sana cha madini ya chuma (iron) na kopa ambayo yanahusika kwa kiasi kikubwa na uwezeshaji wa usambaza wa hewa ya oksijeni mwilini. Kupatikana kwa madini ya chuma na kopa kwenye uyago ni jambo la kipekee ambalo linafanya mmea huo kuwa tofauti na muhimu. Uyoga una Utajiri wa Vitamini B Zikifafanuliwa nguvu za uyoga (Mushrooms) kwa mapana, inaelezwa kuwa Vitamin B2 inayopatikana kwenye uyoga, ni tiba tosha kwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kichwa unaojulikana kama ‘kipanda uso’. Kiasi kidogo cha uyoga utakachokula kitapunguza kasi ya kuumwa kichwa hicho. Vilevile Vitamin B inasifika kwa uwezo wake wa kuzuia uchovu wa m...

Picha: Waziri Ali Abeid Karume awasili Songwe

Image
Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Balozi Ali Abeid Karume amewasili mkoani Songwe akiwa ameambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde kwa lengo la kuandaa na kukagua maandalizi ya mbio za mwenge ambazo kitaifa zinazinduliwa mkoani humo, tarehe 2, April mwaka huu. Wakiwa mkoani humo wametembelea baadhi ya sehemu za vivutio kama kimondo cha Mbozi ambacho ni fahari ya mkoa huo.

Mchekeshaji atajwa kuongoza kura za Urais

Image
Mchekeshaji Volodymyr Zelenskiy(41) anaongoza kwa wingi wa kura zinazoendelea kuhesabiwa nchini Ukraine katika duru ya kwanza ya Uchaguzi wa Rais. Katika kinyang’anyiro hicho yupo pia Rais aliyekuwa madarakani, Petro Poroshenko(53) anayegombea kwa muhula mwingine pamoja na Waziri Mkuu aliyepita, Yulia Tymoshenko(58). Wagombea hawa ni wale wenye maoni yanayoegemea upande wa Umoja wa Ulaya huku wale wenye maoni yanayoegemea upande wa Urusi wakiangukia pua Jumla ya wagombea ni 39, ambapo watatu tu ndio wenye matumaini ya ushindi. Endapo hakuna mgombea atakayepata zaidi ya aslimia 50 ya kura, wawili wanaoongoza watachuana katika duru ya pili Aprili 21, 2019 Endapo Zelenskiy atashinda Urais, atakuwa amebadili kipindi chake cha utani ambapo raia wa kawaida anakuwa Rais baada ya kupambana na rushwa kuwa uhalisia

Israel yavifungua vivukio vya mpakani na Gaza

Image
Israel imevifungua tena vivukio kwenye mpaka wake na Ukanda wa Gaza, licha ya uhasama wa hivi karibuni.  Vivukio hivyo vilifungwa kufuatia mashambulizi ya makombora yaliyoharibu nyumba na kuwajeruhi watu katikati mwa Israel.  Usiku wa kuamkia leo Jumapili, wapalestina wamevurumisha makombora mengine ndani ya Israel, na Israel ikajibu kwa mashambulizi ya vifaru yaliyovilenga vituo vya kundi la Hamas.  Duru za vyombo vya habari zinaarifu kuwa watu wanne wamekwishauawa na mamia kujeruhiwa katika makabiliano hayo tangu Ijumaa iliyopita.  Uamuzi wa kufungua upya vivukio vya kuingia Gaza umefikiwa kufuatia juhudi za upatanishi za Misri. Israel haikusema lolote kuhusu ripoti za upatanishi huo.